Language 

Updates  | Medjugorje[EN]  | Messages  | News & Articles[EN]  | Videos[EN]  | Pictures & Photos[EN] | Site Map  | About[EN]

www.medjugorje.ws » PDA version » Our Lady of Medjugorje Messages » Monthly Medjugorje Messages

Monthly Medjugorje Messages

Wanangu wapendwa! Kwa kuwapenda ninyi, Mungu alinituma kati yenu ili kuwapenda ninyi na kuwasihi katika sala na uongofu, kwa ajili ya amani ndani yenu, katika familia zenu na katika dunia. Wanangu, msisahau kwamba amani ya kweli huja tu, kwa njia ya maombi, kutoka kwa Mungu ambaye ndiye amani yenu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
Wanangu wapendwa! Leo maombi yangu pamoja nanyi ni kwa ajili ya amani. Mema na maovu yanapigana na kutaka kutawala duniani na katika mioyo ya watu. Muwe watu wa matumaini, maombi na imani kubwa kwa Mungu Muumba ambaye kwake yote yanawezekana. Wanangu, amani na itawale ndani yenu na karibu nanyi. Ninawabariki kwa baraka yangu ya kimama ili, wanangu, muwe furaha kwa wale wote mtakaokutana nao. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
Wanangu wapendwa! Kwa furaha nimewachagua ninyi na ninawaongoza kwa sababu ndani yenu, wanangu, ninaona watu wa imani, matumaini na maombi. Wanangu, fahari ya kuwa wangu iwaongoze, nami nitawaongoza kwake Yeye aliye njia, na kweli na uzima. Mimi pia nipo pamoja nanyi ili amani iweze kushinda ndani yenu na kuwazunguka maana Mungu alinituma kwenu kwa nia hii. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
Wanangu wapendwa! Nafurahi pamoja nanyi na namshukuru Mungu kwa kunijalia kuwa nanyi ili kuwaongoza na kuwapenda. Wanangu, amani iko hatarini na familia inashambuliwa. Ninawaalika, wanangu, rudi kwenye sala ya familia. Wekeni Maandiko Matakatifu mahali panapoonekana na msome kila siku. Mpendeni Mungu kuliko vitu vyote ili muwe salama duniani. Asanteni kwa kuitikia wito wangu”.
Wanangu wapendwa! Katika wakati huu wa neema ninawaalika ninyi kuomba kwa moyo wenu. Wanangu, tengenezeni vikundi vya maombi ambavyo ndani yake mtahimizana kutenda mema na kukua katika furaha. Wanangu, bado mko mbali. Kwa hiyo, daima ongokeni upya na mchague njia ya utakatifu na matumaini ili Mungu awape amani kwa wingi. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
Wanangu wapendwa! Nipo pamoja nanyi kuwaambia kuwa nawapenda na ninawasihi sana muombe maana shetani ana nguvu na kila siku nguvu zake zinazidi kuimarika kupitia wale waliochagua kifo na chuki. Ninyi, wanangu, muwe maombi na mikono yangu ya upendo iwanyooshee wote walio gizani na kuitafuta nuru ya Mungu wetu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
Wanangu wapendwa! Katika wakati huu wa neema, ombeni pamoja nami ili mema yapate kushinda ndani yenu na karibu nanyi. Hasa, wanangu, ombeni kwa umoja na Yesu katika njia yake ya msalaba. Wekeni katika maombi yenu ubinadamu huu unaotangatanga bila Mungu na bila upendo wake. Muwe maombi, muwe mwanga na mashahidi kwa wale wote mnaokutana nao, enyi wanangu, ili Mungu wa rehema awarehemu.. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
Wanangu wapendwa! Salini na mfanye upya moyo wenu ili lile jema mlilopanda lizae matunda ya furaha na ushirika na Mungu. Magugu yamechukua mioyo mingi na imekuwa tasa. Kwa hiyo ninyi, wanangu, muwe mwanga, upendo na mikono yangu iliyonyoshwa katika ulimwengu huu unaomtamani Mungu ambaye ni upendo. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
Wanangu wapendwa! Wakati huu uwe wakati wa maombi.
Wanangu wapendwa! Ninawaletea Mwanangu ili aijaze mioyo yenu amani kwa sababu Yeye ni amani. Wanangu, mtafuteni Yesu katika ukimya wa mioyo yenu ili azaliwe upya. Ulimwengu unamhitaji Yesu, hivyo wanangu, mtafuteni kwa maombi maana anajitoa kila siku kwa kila mmoja wenu.
Mama yetu alikuja leo akiwa amevalia mavazi ya heshima akiwa na mtoto Yesu mikononi mwake. Yesu alinyoosha mkono wake kama ishara ya baraka na Mama yetu alituombea kwa lugha ya aramaika.
Wanangu wapendwa! Wakati huu na uunganishwe na sala kwa ajili ya amani na kwa matendo mema ili kusudi ionekane furaha ya kumngoja Mfalme wa amani mioyoni mwenu, ndani ya familia zenu na katika ulimwengu ambao hauna matumaini. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
Wanangu wapendwa! Pepo za uovu, chuki na wasiwasi huvuma duniani kote kuharibu maisha yote. Kwa hiyo Aliye Juu amenituma kwenu ili niwaongoze kwenye njia ya amani na ushirika na Mungu na wanadamu. Ninyi, wanangu, ni mikono yangu iliyopanuliwa: ombeni, mfunge na toeni sadaka kwa ajili ya amani, hazina ambayo kila moyo unatamani. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
To compare Medjugorje messages with another language versions choose
1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 Next>>

 

PC version: This page | Medjugorje | Apparitions[EN]  | Our Lady of Medjugorje Messages  | Medjugorje News & Articles[EN]  | Pictures & Photos[EN]  | Medjugorje Videos[EN]