Our Lady of Medjugorje Messages
Languages:
English,
Afrikaans,
العربية,
Български,
Беларуская,
Català,
Čeština,
Deutsch,
Español,
Français,
Hrvatski,
Italiano,
Kiswahili,
Latviešu,
Magyar,
Malti,
Nederlands,
Norsk,
Polski,
Português,
Română,
Русский,
Shqip,
Slovenčina,
Slovenščina,
Suomi,
Svenska,
Tagalog,
Tiếng Việt,
Українська,
زبان_فارسی
“Wanangu wapendwa! Hata leo - wakati Mungu ameniruhusu kuwaleteeni mtoto Yesu, mfalme wa amani, ili awajaze kwa shauku ya upendo na amani, ili kila moyo uwe kama moyo wake katika wakati huu wa neema - iweni watetezi jasiri wa upendo wa Mungu wenu, ili awape amani yake katika wakati huu wa neema. Asanteni kwa kuitikia wito wangu. ”
“Wanangu wapendwa! Katika wakati huu wa neema, ninawaalika mnifuate. Waombeeni wale ambao hawaombi na hawatamani amani na furaha ambayo ni Aliye Juu pekee anayeweza kutoa. Nafsi zenu ziungane katika furaha ya kusubiri, na mioyo yenu itajazwa amani. Mtasadikishwa, watoto wadogo, kwamba yote yatakuwa sawa na kwamba Mungu atabariki kila kitu, kwa sababu mema mtakayofanya yatawarudieni, na mioyo yenu itajazwa furaha kwa sababu mko pamoja na Mungu na ndani ya Mungu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu. ”
“Wanangu wapendwa! Aliye Juu Zaidi, kwa wema wake, amenipa niwaongoze katika njia ya amani. Wengi wameitikia na wanaomba, lakini kuna wengi ambao hawana amani na hawajamjua Mungu wa upendo. Kwa hivyo, wanangu, salini na pendeni, fanyeni vikundi vya maombi ili kuwahimiza wengine kutenda mema. Mimi nipo pamoja nanyi na ninaomba kwa ajili ya uongofu wenu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu. ”
“Wanangu wapendwa! Wakati huu uwe kwenu wakati wa maombi ya amani. Asanteni kwa kuitikia wito wangu. ”
“Wanangu wapendwa! Wanangu, wapenzi wangu! Mmechaguliwa kwa sababu mmeitikia, mmeweka maelekezo yangu katika vitendo, na mnampenda Mungu zaidi ya yote. Kwa hiyo, wanangu, ombeni kwa moyo wote ili maneno yangu yapate kutimia. Fungeni, toeni sadaka, pendeni kwa upendo wa Mungu aliyewaumba, na muwe, wanangu, mikono yangu iliyonyooshwa kwa ulimwengu huu ambao haujapata kumjua Mungu wa upendo. Asanteni kwa kuitikia wito wangu. ”
“Wanangu wapendwa! Katika wakati huu wa neema, ambao Aliye Juu ameniruhusu niwapende ninyi na kuwaongoza kwenye njia ya utakatifu, Shetani anataka kuwatia ninyi kwa kamba ya kutotulia na chuki. Msimruhusu ashinde, bali piganeni, wanangu, kwa ajili ya utakatifu wa kila maisha ya mwanadamu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu. ”
“Wanangu wapendwa! Pia leo namshukuru Mwenyezi kwa kuwa pamoja nanyi na kuweza kuwaongoza kuelekea kwa Mungu wa upendo na amani. Itikadi zinazowabomoa ninyi na maisha yenu ya kiroho ni za mpito. Ninawaita ninyi wanangu, mrudieni Mungu kwa maana kwa Mungu mnayo wakati ujao na uzima wa milele. Asanteni kwa kuitikia wito wangu. ”
“Wanangu wapendwa! Katika wakati huu wa neema ninawaalika muwe watu wa matumaini, amani na furaha, ili kila mtu awe mtunza amani na mpenda maisha. Wanangu, ombeni kwa Roho Mtakatifu ili awajaze kwa nguvu za Roho wake Mtakatifu za ujasiri na kuachwa. Wakati huu pia utakuwa zawadi kwenu na safari katika utakatifu kuelekea uzima wa milele. Niko pamoja nanyi na ninawapenda. Asanteni kwa kuitikia wito wangu. ”
“Wanangu wapendwa! Upepo wa kutotulia, ubinafsi na dhambi huteka nyoyo nyingi na kuzipeleka kwenye kutotulia na kuangamia. Kwa hiyo, ninawaalika ninyi, wanangu, mrudi kwa Mungu na kusali ili mpate kuwa na afya njema mioyoni mwenu na katika nchi mnayoishi. Ninawapenda ninyi wanangu, na ndiyo maana sichoki kuwaalika mgeuke. Asanteni kwa kuitikia wito wangu. ”
“Wanangu wapendwa! Katika mwaka huu wa neema ninawaalika kwenye uongofu. Wanangu wapendwa, mtangulizeni Mungu katika maisha yenu na matunda yake yatakuwa upendo kwa jirani na furaha ya kushuhudia; utakatifu wa maisha yenu utakuwa ushuhuda wa kweli wa imani. Asanteni kwa kuitikia wito wangu. ”
To compare Medjugorje messages with another language versions choose