Language 

Updates  | Medjugorje[EN]  | Messages  | News & Articles[EN]  | Videos[EN]  | Pictures & Photos[EN] | Site Map  | About[EN]

www.medjugorje.ws » PDA version » Our Lady of Medjugorje Messages » Our Lady of Medjugorje Messages

Our Lady of Medjugorje Messages

Wanangu wapendwa! Niko pamoja nanyi kuwaongoza katika njia ya uongofu kwa sababu, wanangu, kwa maisha yenu mnaweza kuleta nafsi nyingi karibu na Mwanangu. Iweni mashahidi wenye furaha wa Neno la Mungu na wa upendo, mkiwa na matumaini ndani ya mioyo yenu yashindayo uovu wote. Mwasamehe wanaowadhuru na tembeeni katika njia ya utakatifu. Ninawaongoza kwa Mwanangu ili Yeye awe njia, ukweli na uzima kwenu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
Wanangu wapendwa! Ninafurahi pamoja nanyi na kuwashukuru kwa kila sadaka na sala ambayo mlitolea kwa makusudi yangu. Wanangu, msisahau ya kuwa ninyi ni muhimu katika mpango wangu wa wokovu wa wanadamu. Rudeni kwa Mungu na kwa sala ili Roho Mtakatifu atende kazi ndani yenu na kupitia ninyi. Wanangu, Mimi ni pamoja nanyi hata katika siku hizi ambapo shetani anapiga kwa vita na kwa machukio. Utengano ni wenye nguvu na maovu yatenda kazi katika mwanadamu kama hajatenda bado mpaka leo. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
Wanangu wapendwa! Ninawatazama na ninamshukuru Mungu kwa kila mmoja wenu, kwa sababu ameniruhusu niwe nanyi tena ili kuwasihi katika utakatifu. Wanangu amani inavurugika na shetani anataka mahangaiko. Kwa hiyo maombi yenu yawe na nguvu zaidi ili kila roho chafu ya utengano na vita itulie. Iweni wajenzi wa amani na wachukuaji wa Aliyefufuka ndani yenu na karibu nanyi ili mema yapate kushinda katika kila mtu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
Wanangu wapendwa! Ninasikiliza kilio chenu na maombi ya amani. Shetani amekuwa akipigania vita kwa miaka mingi. Kwa hiyo Mungu amenituma kati yenu ili niwaongoze katika njia ya utakatifu, kwa sababu ubinadamu uko kwenye njia panda. Nawaalikeni: mrudieni Mungu na amri za Mungu mkae vizuri hapa duniani na mtoke katika janga hili ambalo mmeingia kwa sababu humsikii Mungu anayewapenda na anayetaka kuwaokoa na kuwaongoza kuelekea maisha mapya. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
Wanangu wapendwa! Nipo pamoja nanyi na tusali pamoja. Wanangu nisaidieni kwa maombi ili shetani asishinde. Nguvu yake ya mauti, chuki na woga imeitembelea Dunia. Kwa hiyo wanangu, mrudieni Mungu katika maombi na katika kufunga na kuwanyima kwa ajili ya wote waliokanyagwa, maskini na wasio na sauti katika dunia hii pasipo Mungu. Watoto wadogo, msipomrudia Mungu na amri zake, hamna wakati ujao. Kwa hiyo amenituma kwenu ili niwaongoze. Leo ninawaalika mrudi kwenye sala ya kibinafsi. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
Wanangu wapendwa! Leo ninawaalika kurudia sala zenu za binafsi. Wanangu, msisahau ya kuwa shetani ni mwenye nguvu na hutaka kuvuta nafsi nyingi iwezekanavyo kwake. Kwa hivyo, ninyi kesheni katika sala na muwe na azimio katika kutenda mema. Mimi niko pamoja nanyi na ninawabariki nyote kwa baraka yangu ya kimama. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
Wanangu wapendwa! Ninawaletea Mwanangu Yesu awapeni amani yake. Wanangu, bila amani hamna wala wakati ujao, wala baraka, kwa hiyo rudieni kusali kwa sababu tunda la sala ni furaha na imani, na bila hiyo hamwezi kuishi. Baraka ya leo tunayowapa, ileteni kwa jamaa zenu na tajirisheni wote wale mnaokuta ili wahisi neema ambayo mnapokea. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
Wanangu wapendwa! Niko pamoja nanyi katika wakati huu wa rehema na ninawaalika nyote kuwa waleta amani na upendo katika ulimwengu huu, ambapo, wanangu, Mungu anawaalika kupitia Kwangu kuwa sala, upendo na kielelezo cha Paradiso, hapa duniani. Mioyo yenu na ijazwe na furaha na imani katika Mungu ili, wanangu, muwe na imani kamili katika mapenzi yake matakatifu. Hii ndiyo sababu mimi niko pamoja nanyi kwa sababu Yeye, Aliye Juu, ananituma kati yenu ili kuwahimiza ninyi kuwa na matumaini na mtakuwa waleta amani katika ulimwengu huu wenye wasiwasi. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
Wanangu wapendwa! Rudieni kusali maana wanaosali hawaogopi wakati ujao. Wale wanaosali wako wazi kwa uzima na wanaheshimu maisha ya wengine. Yeyote anayesali, wanangu, anahisi uhuru wa wana wa Mungu na kwa moyo wa furaha hutumikia kwa manufaa ya ndugu yake. Kwa sababu Mungu ni upendo na uhuru. Kwa hiyo, wanangu, wanapotaka kuwafunga kwa minyororo na kuwatumia hilo halitoki kwa Mungu maana Mungu ni upendo na humpa kila kiumbe amani yake. Kwa hiyo amenituma niwasaidie ninyi kukua katika njia ya utakatifu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
Wanangu wapendwa! Ombeni, shuhudieni na mfurahi pamoja nami kwa sababu Mwenyezi Aliye Juu ananituma tena kuwaongoza katika njia ya utakatifu. Mjitambue, wanangu, kwamba maisha yenu ni mafupi na umilele unawasubiri ili kwamba pamoja na watakatifu wote mmtukuze Mungu kwa nafsi yenu. Msiwe na wasiwasi, wanangu, kwa mambo ya kidunia lakini tamanini Mbingu. Mbingu itakuwa lengo lenu na furaha itatawala moyoni mwenu. Niko pamoja nanyi na ninawabariki nyote kwa baraka yangu ya kimama. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
To compare Medjugorje messages with another language versions choose
<<Previous  1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 ... 23 Next>>

 

PC version: This page | Medjugorje | Apparitions[EN]  | Our Lady of Medjugorje Messages  | Medjugorje News & Articles[EN]  | Pictures & Photos[EN]  | Medjugorje Videos[EN]